Burudani

NINI afunguka kunasa ujauzito wa Nay wa Mitego

Msanii wa muziki Bongo, Nini amefunguka kuhusu kuwa mjamzito.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Niwe Dawa’ amesema si kweli kuwa ana ujauzito wa Nay wa Mitego kwa inavyozungumzwa.

“Hapana, haiwezi kuwa, hamna kitu kama hicho,” amesema Nini.

Kumekuwepo na stori kuwa Nini na Nay wa Mitego wapo katika mahusiano ya kimapenzi tangu kutoa ngoma yao iitwayo Niwe Dawa.

Pia moja ya sababu zilizotajwa kumuondoa Nini MJ Records ni kudaiwa kuwa na mahusiano na Nay wa Mitego, hata hivyo wote wawili wamekuwa wakikanusha hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents