Burudani

Nipo kwenye break kidogo ila nitarudi tofauti – Nisher

Muongozaji wa video kutoka Arusha, Nisher amesema ameamua kupumzika kwa muda ili afanye shughuli za kifamilia pamoja na kujipanga vizuri.

11909937_518920154933584_1087997624_n

Nisher ameiambia Bongo5 kuwa amefanya kazi kwa miaka mitatu bila kupata mapumziko na kuwa karibu na familia.

“Mimi nipo kwenye break kidogo,” amesema. “Unajua nimekimbizana kwa miaka mitatu hivi non-stop bila mapumziko, unakuta unachanganyikiwa. Pia mdogo wangu anajiandaa kuoa sasa ananihitaji kwa ajili ya ushauri na nini. Kwahiyo nitakapokuwa tayari nitarudi tena,” ameongeza.

“Pia nilisafiri Dubai, Afrika Kusini kuangalia location pamoja na connection. Siwezi kusema lini nitarudi ila ni siku yoyote na nitafanya kama surprise hivi. Unajua mwanzoni nilivyoanza nilikuwa kama nyota hivi kila siku unaiona ila safari hii napotea lakini nitarudi kama kimondo. Nataka nifanye kama historia, sasa hivi siangalii kufanya kazi kama watu wengine wanavyofanya kama karanga, kazi kila wakati No! Nataka chochote nachokifanya kikae na watu kichwani kwa muda mrefu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents