Michezo

Nipo tayari kwenda Real Madrid – Hazard

Mchezaji wa mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, Chelsea Eden Hazard amesema yupo tayari kutua katika klabu ya Real Madrid kama watawasilisha dau nono.

Mchezaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard akiwa amebeba Kombe la Ligi kuu nchini Uingereza 2017

Hazard amekuwa akihusishwa sana kutua katika kikosi cha kocha Zinedine Yazid Zidane “Zizou” ambao ni mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya, hata hivyo mchezaji huyo ameumia katika kifundo cha mguu wakati wa mazoezi na timu ya taifa ya Ubelgiji

Akizungumza na chombo kimoja cha habari alisema “Sote huwa tuna ndoto. Inaweza ikawa Hispania, lakini pia si ajabu ni kisalia Chelsea,”

Mchezaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard akihusishwa na kuhamia Real Madrid

“Tusubiri tuone maana si jambo ambalo nalifikiria kwa sasa ”
Hazard aliongeza: “Ikitokea kwamba nimehamia Real Madrid,upo uwezekano pia wa kwenda kusugua benchi, hivyo nahitaji kuwa namaamuzi sahihi “.

Kijana huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26, alitua Chelsea akitokea katika klabu ya Lille ya nchini Ufaransa mwezi Juni 2012.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuihama Chelsea, alisema: “Katika soka, huwezi ukajua, lakini sasa hilo halimo akilini mwangu.

“Mimi ni mchezaji wa Chelsea. Bado nina kandarasi ya miaka mitatu hapa”

BY HAMZA  FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents