Videos

Nisher aendelea kutisha kwenye video ya wimbo wa Feza Kessy ‘Amani ya Moyo’

Ikiwa ni siku chache tu baada ya kuachia video ya Ben Pol iliyopokelewa vizuri na mashabiki wa muziki nchini, muongozaji wa video hiyo, Nisher ameendelea kutisha zaidi baada ya jana kuachia video ya wimbo wa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, The Chase, Feza Kessy uitwao ‘Amani ya Moyo’.

http://youtu.be/nK6KVwe_tMk

Watu wengi wameisifia video hiyo wakidai kuwa Nisher ameongeza kitu kikubwa kwenye video za muziki za Tanzania ambazo nyingi huishia kuchezwa hapa hapa nchini.

“Daah Huyu Nisher aliyefanya video ya Ben Pol yuko vizuri sana!nimeona video ya @FezaKessy nayo amefanya yeye, ni kufuru,” ametweet muigizaji wa filamu Elizabeth Michael aka Lulu.

Naye Jokate Mwegelo ā€¸ameisifia video hiyo kwa kuandika: Awesome job again my friend. She looks great!!

Waongozaji wengine wa video nchini wanapaswa kujifunza kwa Nisher jinsi anavyotumia mitandao ya kijamii kutangaza kazi zake na kuwasiliana vizuri na mashabiki.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents