Burudani

Nisher awajibu wanaomdiss kwenye wimbo mpya ‘Paper’ leo ni siku yake ya kuzaliwa

Director wa video nchini Nisher, ameachia single yake mpya iitwayo ‘Paper’ kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Kwenye wimbo huo wa R&B aliouproduce mwenyewe, Nisher anasema na haters wake ambao wamekuwa wakimkatisha tamaa licha ya kukubalika nchini hasa baada ya kufavya video ya Jikubali ya Ben Pol. Hivi karibuni Nisher alidai kuwa watu wa Arusha wamekuwa wakimkatisha tamaa.

“Huu ni wivu tu mafanikio ni lazima, kwenye media kila saa sasa wanamuona Nisher,and am not stopping man, Got ma mind on ma paper,”anasikika akiimba Nisher kwenye wimbo huo.

“Salama kwenu haters na wote mnaodiss, you can join my crew or you can suck my ……. business. Hata usipopenda, demu wako ananipenda nampa vile roho yake inapenda anasema damn.”

Nisher hakusita pia kuimba kuhusu maisha safi aliyonayo na kwamba anachowaza ni kuendelea kutafuta ‘paper’.

“Akili kwenye karatasi, napanda ndege sio basi.”

Kingine alichosema ni nini………. Okay ameipa shoutout Bongo5 kwenye wimbo huu. Thanks Nisher.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents