Michezo

Nitaachana na McLaren- Alonso

Dereva wa kampuni ya McLaren-Honda, Fernando Alonso ameonyesha nia ya kutaka kuondoka katika kampuni hiyo kama haitaonyesha ushindani katika mashindano ya Formula 1 ya mwezi Septemba mwaka huu.

Dereva wa Fomular 1,Fernando Alonso 

Bingwa huyo wa dunia mara mbili mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Nilazima tushinde, Kama tutashinda kabla ya mwezi Septemba, nitafanya maamuzi ya kusalia. Nilijiunga hapa ili kushinda mataji na kama hatutakuwa na ushindani nitachukua jukumu la kuondoka. Hadi nitakapo kaa chini na kujitasmini mwenyewe na hivyo sitakuwa na uhakika juu ya hilo,” amesema.

Dereva wa Fomular 1,Fernando Alonso 

Mhispania huyo mpaka sasa bado hajafanya maamuzi juu maisha yake ya baadae ndani ya timu hiyo.
Alonso alijiunga na McLaren mwaka 2015 wakati alipoanza mahusiano yake na mmoja kati ya mafundi wa kampuni hiyo, lakini timu hiyo imeonekana kuwa katika hali mbaya kwa miaka mitatu sasa.

Mashabikiwa dereva,Fernando Alonso ni miongoni mwa madereva maarufu katika Fomular 1

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents