Habari

Nitagombea Urais 2020 nikipewa ridhaa na Chadema – Tundu Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu ametangaza nia ya kutaka kuwania Urais Tanzania mwakani iwapo chama chake kitaridhia.

Tundu Lissu ambaye kwa sasa anatibiwa nchini Ubelgiji baada ya kujeruhiwa kwa risasi mwaka 2017 amesema vikao vya chama ndiyo vitatoa mwelekeo wa nani atasimama mwaka 2020.

“Inawekana kabisa wanachama wenzangu na viongozi wakasema bwana Lissu hautoshi nitakubaliana nao, wanaweza wakasema Mzee Lowassa hebu muachie huyu kijana mapambano ni makali zaidi yanahitaji nguvu mpya, nitasimama” Lissu alisema hayo akizungumza na Zuhura Yunus mjini London katika kipindi cha BBC cha HardTalk.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents