Habari

Nitahakikisha shule zote za Dar zinakuwa na umeme – RC Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda Jumatano hii alikuwa na mkutano na walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na wadau wa elimu ndani ya mkoa huo kujadiili changamoto mbalimbali pamoja na kuzitolea ufumbuzi.

Katika mkutano huyo uliofanyika katika ukumbi wa ICC  jijini Dar es salaam,  walimu wa msingi na sekondali pamoja na maafisa elimu kata walipata fursa ya kuzungumza changamoto ambazo zinawakabili katika maeneo yao ya kazi hali inayosababisha ufaulu kuwa mdogo.

Baadhi ya changamoto ambazo zilitajwa na walimu hao ni pamoja na ukosefu wa fensi za shule, uchakavu wa maradara, ukosefu wa vyoo, upungufu wa waalimu, shule kutokuwa na umeme pamoja na utoro mashuleni.

Akiongea katika ukumbi huo muda mchache baada ya kero hizo kuhainishwa,  Mkuu huyo amesema ofisi yake itaanza mara moja ukarabati wa shule zote pamoja na kuanza kujenga vyoo katika shule ambazo zinachangamoto hiyo.

“Suala la vyoo, bati kwa kwaajili ya kupaua shule zote ambazo zinauchakavu naomba muwasiliane na ofisi ya mkuu wa mkoa na wiki ijayo tutaanza kutoa bati ili ukarabati uanze mara moja. Rais wetu John Pombe Magufuli ametaka watanzania wasome bure na tayari wanafunzi wanasoma bure na changamoto tulizo nayo ndio tunapambana nazo sisi wasaidizi wake, kwa namna hiyo ili kuhakikisha elimu ndani ya mkoa wangu inakuwa bora na ufaulu uwe juu kwa sababu tukiizungumzia Dar es salaam hiki ni kitovu cha Tanzania, tunaangaliwa kama mfano na kila kosa sasa ni lazima tuweke mambo sawa na tuwe mfano,” alisema RC Makonda.

Aliongeza,”Umeme unakuwa historia muda mchache ujao katika shule zetu kwa sababu umeme wa gesi tayari umeingia ndani ya Dar es salaam. Nitahakikisha shule zote za Dar zinakuwa na umeme, siwezi kuwa RC wa Dar halafu shule zangu zinakosa umeme. Bila shaka hii itakuwa ni chachu ya maendeleo katika sekta ya elimu,  kwahiyo wale waalimu ambao walikuwa wanalalamika suala la umeme siku chache zijazo itakuwa historia,”

Pia mkuu huyo aliwataka watumishi wa umma katika sekta ya elimu kuhakikisha wanawajibika ipasavyo katika majukumu yao ili kubadili ya matokeo ya ufaulu katika jiji la Dar es salaam na kutoa taswira mpya kwa mikoa mingine.

Pia katika mkutano huo, Afisa elimu mkoa wa Dar es salaam Hamisi Lissu aliwatumbua maafisa elimu 12 aliokuwa wanadai nyongeza ya posho nje ya mshahara wakidai laki mbili na nusu wanayopewa haitoshi huku wenzao 16 wakipingana na suala hilo hali iliyompelekea mkuu huyo kuwaengua na kuwatafutia kazi nyingine yakufanya.

Katika hate nyingine RC Makonda alisema katika sekta ambayo mpaka sasa inaenda vizuri ndani ya mkoa wake wa Dar es salaam ni afya baada ya hivi karibuni kuzindua wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam yenye uwezo wakuchukua wangojwa zaidi ya 150.

<img class=”alignnone size-full wp-image-196910″ src=”http://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/07/Unknown-2.jpg” alt=”” width=”640″ height=”426″ />
<strong>Jengo la wodi ya akina na watoto.</strong>

Pia ujenzi wa wodi kama hizo unaendelea katika hospitali ya Mwananyamala pamoja na Temeke ambazo zote kwa pamoja zitakuwa zinachukua vitanda 450.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents