Michezo

“Nitahamia ligi ya Uhispania ili nishide tuzo ya Ballon d’Or” – Hazard

Aendelea kuwaweka roho juu mashabiki wa Chelsea

Mchezaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard, anaendelea kuwaweka roho juu mashabiki wa klabu ya Chelsea baada ya kueleza matakwa yake ya kutaka kuhamia ligi ya Uhispania Laliga.

Mchezaji huyo ameongea hayo wakati akiongea na Skysport akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na kueleza nia yake yote jinsi anavyojichukulia yeye mwenyewe.

Hazard pia aliongeza baada ya kuulizwa wewe ni mchezaji bora duniani kwa sasa ? alijibu ” Ndio mbona nilishaongea kipindi cha nyuma ila naongea tena”

Baada ya kuulizwa kuwa “Kushinda tuzo ya mchezaji bora duniani Ballon d’Or kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita ni lazima ucheze ligi ya Uhispania” Hazard alijibu ” Labda ndio maana nataka kuhamia huko” akaulizwa muda wa kwenda huko “Utaenda mwezi januari ?” akajibu “Hapana”

Lakini pia hakuishia hapo baada ya kuulizwa kuhusiana na kiwango chake “Je utaendelea kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani ? alijibu ” Kila mara uwezo wa kufunga na kutoa msaada wa magoli utaongezeka ingawa wachezaji wenzangu katika timu wamenisaidia sana ila na mimi ntajitahidi kuonyesha uwezo kila mara ”

Imekuwa muda sasa mchezaji huyu kuhusishwa na tetesi za kujiunga na klabu ya Real Madrid kutoka Uhispania baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika Ingawa mchezaji mwenzake wa Ubelgiji na aliyekuwa mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois ambaye tayari amejiunga na miamba hiyo ya Uhispania Real Madrid.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents