Michezo

Nitakuwa nje ya ulingo mpaka lini ? – Tyson Fury

Mwanamasumbwi wa uzito wa juu duniani raia wa Uingereza, Tyson Luke Fury ameomba kufutiwa adhabu yake ya kutoshiriki mchezo wa ngumi baada ya kuwa nje ya ulingo takribani mwaka mmoja sasa.

Mara ya mwisho, Fury aliingia ulingoni mwezi Novemba mwaka jana alipopambana na Wladimir Klitschko. Mahakama ilisogeza mbele kusikilizwa kwa kesi yake na mpaka sasa bado haijapangwa tena.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Fury ameandika kuwa “Nitaendelea kusubiri kwa muda gani hadi kurejea tena?”

Fury ameongeza “Nimekuwa nje ya mchezo huu kwa mwaka mmoja na miezi mitatu sasa tangu niwechini ya uchunguzi”.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 29 anasubiri kuhojiwa na bodi ya kuzuia matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni kisha kutolewa maamuzi ya kesi yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents