Michezo

Nitalipa mishahara ya wachezaji mwaka mzima – January Makamba

Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba amewaahidi mashabiki, wanachama na viongozi wa klabu ya Coastal Union kulipa mishahara ya wachezaji wa timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Makamba ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Costal Union dhidi ya timu ya Mbeya kwanza uliyopigwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani Septemba 17 mwaka huu ambapo Costal ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

“Kwaimani yangu siku ya leo ambayo ni mepata bahati ya kuhudhuria mchezo huu ambapo timu yetu sasa inataka kurudi kwenye enzizake, imaniyangu ni kwamba safari hiyo itakamilika vizuri”, amesema hayo Makamba kupitia Azam Tv baada ya kumalizika kwa mchezo wa Costal dhidi ya Mbeya kwanza.

Makamba ameongeza “Mimi kama mshabiki wa Costal lakini kama kiongozi wa Tanga nimewaambia viongozi wa timu kwamba miaka yote kunakuwa na shida sijui mshahara, chakula, safari na kadhalika”.

“Sasa mimi nasema kwa sababu leo ni siku nzuri kwa wachezaji wote wa Costal Union katika mwaka mzima kuanzia sasa hawatakosa mshahara mwezi hata mmoja na hawatokosa chakula na hawatoshindwa kusafiri”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents