Michezo

Nizar Njia Panda Stars

Kiungo wa Taifa Stars Nizar Khalfani yupo katika hatihati ya kuichezea timu hiyo kwenye michuano ya chalenji kutokana na kukabiliwa na majukumu katika klabu yake ya Vancouver Whitecaps ya Canada, ingawa amebainisha kuwa anasubiri hadi mwisho wa wa wiki hii kujua mustakabali wake.

Kocha wa Taifa Stars Jan Poulsen tayari ameshatangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 jijini Dar es salaam na amewajumuisha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi akiwemo Nizar, Herry Joseph na Mrwanda.

‘Bado sijajua kama nitakuja,kwani bado nina majukumu na timu yangu na nasubiri kwanza ruhusa ya wakuu ndipo nijue kama nitaweza kujiunga na Taifa Stars,’ alisema Nizar.

Wakati huo huo Danny Mrwanda alisema atatua Jumamosi au Jumapili tayari kwa michuano hiyo na amedai atajituma vilivyo kuhakikisha anatwaa ufungaji bora. Henry Joseph anatarajiwa kutua wiki ijayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents