Michezo

Nje ya kikapu huu ni mchezo mwingine Stephen Curry anaoupenda (+Video)

Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kutoka Marekani, Stephen Curry ameonesha mahaba ya mchezo mwingine nje ya kikapu ambao anaupenda na pengine huenda alishawahi kuwa na  ndoto ya kucheza mchezo huo nao ni mpira wa miguu.

https://youtu.be/TaiBZq5WbVU

Stephen Curry ambaye wikiendi iliyopita alipata nafasi ya kutembelea klabu ya Chelsea, alionekana akipiga penati na kufanya mazoezi madogo madogo huku akiwa mwenye furaha kwa kuonesha mahaba yake kwenye mchezo huo.

Mashabiki wengi wa klabu ya Chelsea wameonesha kufurahia ujio wake, Stanford Bridge huku wengine wakimpongeza kwa kupiga nzuri.

https://twitter.com/irfan7ali/status/909550504342167554

 

Nyota huyo wa NBA anaekipiga kunako klabu ya Golden State Warriors ambaye yupo kwenye mapumziko mwezi uliopita alikuwa nchini Ufaransa na kuhudhuria kwenye mchezo kati ya PSG dhidi ya St Etienne, hii ni ishara tosha kuwa huenda Curry anavutiwa sana na mpira wa miguu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents