Habari

Njia 15 za kumfanya ‘Mteja’ awe ‘Teja’ wa huduma yako

By Mark Rose Msemwa

Katika maisha ni lazima pande hizi mbili uzitumikie, kuwa kuna wakati utakuwa mteja na kuna wakati utakuwa mhudumu, iwe unajua au hujui ila hivyo ndivyo ilivyo na huna namna ya kukwepa ilhali ungali hai hata ungekuwa Mhadzabe, daktari, mwalimu, mke, mume, handsome, mrembo n.k…..

SA-image-business-woman-2

Ni siku nyingine tena ambapo nakutana nawe kupitia maandishi kwa lengo lakukuza upeo wetu. Leo nimeona ni vema nikushirikishe katika njia hizi ambazo zimenisaidia mimi kutoka kwenye malipo ya 3,000 elfu tatu kwa mwezi kwa kazi za shamba hadi 1,700,000 milioni moja na laki saba kwa mwezi kwa kazi ya kutengeneza kucha, hapa hapa Tanzania nchi yangu ya amani.

Sina chanzo kingine juu ya mada hii zaidi ya uzoefu wangu niliojaaliwa na Muumba; Kama nimeweza basi naamini nawe unaweza pia, popote ulipo duniani una uwezo wa kuzitumia na zikakupa faida kubwa mno;

1; Penda kazi yako hata kama unaifanya katika mazingira magumu. Kuna mbinu moja tu ya kukufanya uipende kazi yako hata kama ulikuwa huipendi na pengine si chaguo lako, ni kwa kuangalia kazi yako ina umuhimu gani kwako. Kama haina umuhimu wowote acha haraka mno. Mandela alisema, hakuna binadamu anayezaliwa na chuki ila hujifunza, na
hujifunza basi ana uwezo wa kujifunza kupenda pia.

2; Jijali na kuwa nadhifu. Wataalam wengi wa biashara husema moja ya mbinu kubwa ya huduma kwa mteja ni kauli nzuri, je vipi kama kauli nzuri inatoka kwenye kinywa kichafu, hakijapigwa mswaki tena kwa mtu anaye nuka kwapa?
Ukijijali wewe ndipo utakuwa na uwezo wa kumjali mtu mwingine akiwemo mteja. Unadhifu ni nguzo ya kwanza hata kwenye usaili wa kazi yeyote.

3; Mjali mteja kwa uteja wake na sio, cheo, umaarufu wala utajiri alionao, mbwembwe zote alizo nazo ni mali yake na kwako kaja kufuata huduma yako, na analipa bei sawa na wengine. Kwanza watu wa hadhi ya juu wengi wao huwa hawataki kunyenyekewa na kubabaikiwa wakiwa nje ya kazi zao.

4; Usifikirie pesa wakati wa kumhudumia mteja, mfano mshahara au tip, jali huduma yako kwanza pesa itafuata ubora wa huduma yako. Fatuma Karume alisema; Baba yetu alikuwa anatuambia, tujitahidi kadiri tuwezavyo kuwa bora katika
huduma za taaluma zetu na watu watawekeza fedha katika huduma hizo. This works.

5; Usianzishe mazungumzo ya nje ya taaluma yako na huduma yako kwa mteja usiyemjua, (marufuku) unaweza ukaongelea watoto ukashangaa mtu anaangua kilio, unaweza ukaongelea siasa kumbe ni hasimu, mwache mteja aanze wewe kuwa
supporter. Labda kama unamjua vizuri na usijiroge ukamkopa mteja wako sumu. Pia usilete mazoea always kumbuka yeye ni mteja hata mtaniane vipi!….

Itaendelea…..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents