Habari

NJia tano za kugundua kuwa mpenzi wako ana Msongo wa Mawazo

Watu wengi wanapatwa na hali ya kukosa raha au kushuka moyo wanapokuwa wameghafirika au kukosa msaada wa kitu fulani. Wakiwa na msongo wa mawazo au wanapata changamoto ya ya maisha katika kitu fulani.

didnt-get-promotion

Mara nyingine ni hali ya familia haijakaa sawa, kazi nyingi ofisini, hali ya kifedha au kufiwa na mtu aliyempenda sana na ambaye alikuwa akiwapa msaada mkubwa lakini hayo yote yanatakiwa yawe kwa muda fulani halafu maisha yaendelee tena.

Ingawa hali hii ya kushuka moyo inaanza kuisha na kuanzisha kitu kingine kabisa ambacho inaweza kuwa dalili za kupata msongo wa mawazo ulio mkali;

Hapa kuna viashiria vitano ambavyo mwenzi wako au mpenzi wako anaweza kuwa navyo.

Wanaanza kukosa uchangamfu ambao alikuwa nao hapo kabla na anaacha kufurahia vitu ambavyo alizoea kuvifurahia. Watu wenye msongo wa mawazo mkali huwa wanapoteza hamu ya kushiriki vitu walivyokuwa wakivifanya na hata wanaacha kujumuika kwenye jamii, hujitenga na kutopenda kuwa karibu na watu.

Hujiona wameelemewa na maisha, hujiona hawana tena nguvu wala ujasiri na mara nyingine huwa ngumu hata kufanya kazi ndogo ndogo kama kuamuka tu kitandani asubuhi. Huwa wanakuwa wakali na wenye hasira za chap chap huku kila wakati wakitafuta makosa juu yao wenyewe au kwa watu wengine.

Hawawezi kuzingatia jambo na kwasababu ya kushuka moyo wanakuwa wanakera. Hivyo huanza kuonyesha dalili za mtu ambaye amekata tamaa ya maisha na wakati mwingine kuzungumzia habari za kujiua. Kama unaona dalili ya mojawapo ya vitu hivyo kwa mwenzi wako chukua hatua ya kuanza kushughulika naye ili kumsaidia kutoka hapo alipo.

Watu ambo wameshuka moyo huwa ni vigumu kugundua kwamba wanahitaji kupata msaada ila kwa taarifa sahihi na kuwajali kushuka moyo kunatibika.

Kushughulikia hali hiyo ya kushuka moyo kunaweza kuwa changamoto ukiwa unashughulikia peke yako. Kwasababu hiyo unahitaji wataalamu wa kisaikolojia na magonjwa yanayohusika na kushuka moyo au msongo wa mawazo. Kushuka moyo na msongo wa mawazo kunatibika na wataalamu wenye elimu ya saikolojia ya mazingira, kupona kwake kunaweza kufanikiwa kama dalili na matatizo yanayosababishwa yatashughulikiwa ipasavyo.

Uchunguzi wa hivi karibuni unasema ya kuwa ili tiba kwa mtu aliyeathiriwa na kushuka moyo au msongo wa mawazo inapaswa wana familia kuhusishwa na kuelimishwa ili waweze kutoa msaada wa kutosha kwa mwathirika.

Endapo utagundua hali hiyo ni vizuri kutafuta daktari anayehusika na kumwelezea kitu ambacho mpendwa wako anapitia na kutafuta namna mpya ya kuishi kushughulikia uwezo wa kufikiri, hisia pamoja na tabia kwa ujumla wake.

Chanzo cha makala hii ni kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia ya magonjwa yanayotokana kushuka moyo na Msongo wa Mawazo

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents