DStv Inogilee!

Njia za kukusaidia kufanya mabadiliko hata kama kubadilika ni kazi ngumu

Viongozi wazuri huweza kushughulikia mabadiliko vizuri, iwe kwenye ngazi ya kisiasa, kijamii na hata kibiashara.

Byron-Scott-isnt-even-mad-anymore.-Just-disappointed.-AP

Rais Jonathan anaweza akawa mtu wa kuigwa kwenye siasa za Nigeria kitu ambacho mataifa mengi ya Afrika wanashindwa kufanya na hata yale ya Mashariki ya Kati. Kuna viongozi wao wanadhani wao ndio kila kitu au miungu wadogo lakini ukweli wa mambo ni kila jambo lina wakati wake hivyo kila utawala una wakati wake. Ukijua hivyo  ni rahisi kukabiliana na mabadiliko pale ambapo yanahitajika.

Hizi ni namna nne ya kufanya mabadiliko yenye tija katika taasisi, shirika la kiserikali au dini na hata siasa :

1. Unatakiwa kuwa na taarifa juu ya maendeleo yako na kukaribisha mawazo ya watu wengine yenye msingi. Kujenga katika mabadiliko unahitaji muda ambao utakuwa ukitoa ripoti ya wapi umefikia na kuruhusu mawazo mapya. Hii inahusisha kushirikisha timu yako ya utendaji, kufanya tathmini pamoja na kuandalia ripoti ya utendaji wake ulikwendaje.

Karibisha wahusika wote katika vikao vyenu ili kusiwe na habari ambayo itafika nusu nusu au kutokufika kabisa. Kama mabadiliko hayaendi ilivyotarajiwa, inakubidi uwe mkweli na zingatia ufumbuzi zaidi na wala si tatizo au aliyesababisha tatizo.

Kama kuna ushirikishwaji wa kila sekta katika taasisi, mabadiliko yatakuwa yenye mafaniko makubwa. Watu wengine wakiona kwamba wamehusika katika mawazo na maamuzi inawapa nguvu ya kuwa sehemu ya kusimamia mabadiliko hayo na kujiona ni sehemu ya hayo maamuzi.

2. Lazima ukubali kuwa mabadiliko yanatisha na kuogofya. Wakati unazungumzia namna ambavyo umeweza kutekeleza na namna unavyoendelea kutekeleza vile vile uweke kwenye akili yako kuwa mabadiliko si rahisi kihivyo. Hakikisha huongei na watu katika namna ambayo hawawezi kuelewa unamaanisha nini na madhara yake yatakuwaje?

Je utawajengea mazingira magumu? Wajulishe kuwa hata kwako inatisha na kuogofya kufanya mabadiliko ili kuwaweka katika picha ya pamoja na wewe mwenyewe kwamba huo wakati utapita na mambo yataendela vizuri kama kawaida.

3. Ongea na watu ambao wataathiriwa na mabadiliko hayo. Kuongea nao unawajengea hali ya kisaikolojia kwamba lolote litakalotokea wake tayari kulipokea. Katika uongeaji huu hasa kama kutatokea watu kuachishwa kazi au kuhamishwa kazi, watu wengi wanapenda mazingira waliyoyazoea mara wanapobadilishwa kuvunjika moyo na wengine huchukua muda mrefu kuendana na hali hiyo bali wachache hawaathiriki.

Hivyo kauli kama “tutakwenda kufanya mabadiliko kutokana na sababu zifuatazo…….” labda mfumo mliokuwa mnautumia umeonekana kushindwa katika kutendaji na utekelezaji wake n.k.  Wakati unasema hayo unahitaji kujua watu wanalipokea vipi na uwape taarifa kwa kila kinachoendelea ili kuwaondoa katika sintofahamu.

4. Hakikisha unakuwa pamoja na wanaopinga au kitu kinachozuia mabadiliko. Wengine watashangaa kwanini kuwa pamoja na hicho kitu au mtu huyo? Ili usiweze kufanya makosa ambayo yataharibu mabadiliko na vile vile kuharibu mfumo mzima wa shirika usipojua kitu kinachozuia mabadiliko kinasimamia nini na misingi yake niko kwenye nini? Ni sawa sawa na kupigana na audio ambaye hujui ana silaha gani huku ukitarajia kushinda vita hivyo, unahitaji kujua adui na washirika wake vizuri kabla ya kuingiza agenda zako.

Ndio maana watu hufanya uchunguzi na upelelezi wa mambo fulani kabla ya kwanza kufanya mabadiliko, maana ukikurupuka ni rahisi sana kuharibu heshima na utendaji wako na vile vile unaweza kuathiri kabisa taaluma yako.

Je kitu gani kinakusaidia kufanya mabadiliko na mageuzi makubwa kwenye shirika, taasisi au chama chenu?

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW