Habari

NJOMBE: Baba mbaroni kwa kumbaka binti yake wa kumzaa wa miaka 11

NJOMBE: Baba mbaroni kwa kumbaka binti yake wa kumzaa wa miaka 11

Ezron Ndone mkazi wa Mtaa wa Joshoni Kata ya Mji Mwema mkoani Njombe anadaiwa kumbaka mtoto wake wa miaka 11 anayesoma darasa la 5,kwa kumlaghai mtoto huyo na kuanza kulala naye chumba kimoja, baada ya kumfukuza Mke wake.

Valentina Mkolongo ni Mama mzazi wa mtoto aliyebakwa ambaye pia  ana jumla ya watoto watano amesema kwa muda mrefu amekuwa na mgogoro na mume wake na ikafika wakati akafukuzwa chumbani na kulazimika kuhamia chumba kingine, na moja ya chanzo cha mgogoro ni mama kupinga uhusiano uliokuwa unatia mashaka kati ya Baba na Binti yao wa kwanza mwenye umri wa miaka 11.

Kwa upande wake mtoto ambaye anadaiwa kubakwa na Baba yake mzazi amesema wakati wakulala alikuwa akiwaita yeye na wadogo zake na wakiwa wamelala akawa anatumia muda huo kumbaka.Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamis Issa, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa ambaye ni mfanyabiashara wa Mkaa.

Chanzo Eatv.tv

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents