Habari

Nkurunziza amzungumzia mrithi wa kiti chake cha Urais Burundi, Evariste Ndayishimiye

Kiongozi wa muda mrefu nchini Burundi Pierre Nkurunziza leo amempongeza mrithi wake aliyemteua kwa ushindi mkubwa aliopata katika uchaguzi wa rais, licha ya kuwa upinzani umeapa kuyapinga matokeo hayo mahakamani.

Maafisa wa uchaguzi walimtangaza Evariste Ndayishimiye, jenerali wa zamani wa jeshi aliyeteuliwa na chama tawala cha CNDD FDD kuwa mrithi wa Nkurunziza, kuwa mshindi wa uchaguzi wa Mei 20 kwa kupata asilimia 68.72 ya kura.

”Nampongeza sana rais mteule jenerali Evariste Ndayishimiye kwa ushindi wake mkubwa ambao unathibitisha kuwa idadi kubwa ya Warundi wanakubali miradi na maadili aliyoianzisha,” Nkurunziza ambaye aliamua kutowania kiti hicho baada ya miaka 15 madarakani, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Mgombea wa upinzani Agathon Rwasa, amekuwa wa pili akipitwa kwa mbali amepata asilimia 24.19 ya kura, lakini chama chake cha National Freedom Council CNL, kimeyakataa matokeo hayo, kikidai kuwapo na udanganyifu katika uchaguzi huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents