Habari

NMB: Huduma ya bima kupitia benki hukuza biashara endelevu

Benki ya NMB imesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kukata bima ya biashara zao ili ziwe endelevu kwa kuzilinda dhidi ya hatari (risks) zinazoweza kujitokeza.

Akizungumza katika semina iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 300 wanaounda Klabu ya Biashara ‘NMB Business Club’ ya Mkoa wa Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati wa NMB – Filbert Mponzi, alisema kuwa biashara hukabiliwa na hatari (risk) mbali mbali ambazo kinga yake ni kuzikatia bima. Majanga kama moto, wizi na mafuriko ni baadhi ya hatari zinazozikabili biashara na kudumaza ukuaji endelevu wake.

Ikiwa na matawi 225 nchini kote, NMB inayo nafasi bora ya kufikisha huduma za bima kwa watu wote (wateja wake na wasio wateja wake) popote walipo.

Benki ya NMB inatoa huduma za bima (Bancassurance) katika matawi yake yote 225 nchini kote kupitiaushirikiano wake na kampuni za bima za Sanlam, UAP, Shirika la Bima la Taifa (National Insurance Corporation – NIC), Jubilee, Shirika la Bima la Zanzibar (Zanzibar Insurance Corporation – ZIC) na Reliance.

Kwa ushirikiano na kampuni tajwa, matawi ya Benki ya NMB hutoa huduma za bima za magari, afya, mali za thamani, maisha, hatifungani na kilimo.

Mponzi alikuwa akizungumza katika semina iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 300 wanaounda Klabu ya Biashara ‘NMB Business Club’ ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kwa kupitia huduma ya bima kupitia benki (Bancassurance), Watanzania wanaweza kukata bima na kuomba malipo ya bima pindi hatari zinapojitokeza kupitia matawi yote na NMB nchini kote.

Vilabu vya Biashara vya NMB huwakutanisha pamoja wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao
hupata nafasi ya kuelimishwa juu ya masuala mbalimbali kuhusu biashara zao.

 

Meneja mwandamizi wa huduma ya bima kupitia benki wa NMB, Martine Massawe, aliwaambia
washiriki wa semina hiyo kuwa uwepo wa matawi ya NMB karibu na maeneo yao kunatoa fursa ya wao kupata huduma za bima kwa karibu zaidi.

Mjasiriamali na mshiriki wa semina hiyo ambaye biashara yake iliathiriwa na moto uliounguza sehemu ya Soko la Tegeta Nyuki Jijini Dar es Salaam hivu karubuni – Godwin Rwechungura alitoa ushuhuda wa jinsi Benki ya NMB ilivyomhakikishia kupata fidia ya hasara aliyoipata.

Naye meneja mwandamizi wa huduma za benki kwa njia ya kidijitali wa Benki ya NMB, Tito Mangesho alisema mbali na huduma za bima kupitia benki, taasisi hiyo ya fedha pia hutoa huduma za NMB Mkononi, Mastercard QR Code na nyingine nyingi kupitia kadi ambazo kwa pamoja husaidia kuboresha ufanisi katika biashara.

Kupitia NMB Mkononi, mteja huweza kufanya miamala ya kifedha popote pale alipo kwa kupitia simu ya mkononi.

Mteja pia anaweza kufanya malipo kama vile ya kodi na tozo mbalimbali za serikali moja kwa moja
kupitia simu ya mkononi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents