Habari

Nonini atoa single mpya ‘Zipi Zoo’ aliyomshirikisha Chidi Benz, anahitaji umshauri, je wafanye album pamoja? (Audio)

Rapper wa Kenya Nonini pamoja na rapper wa Tanzania Chid Benz ni washkaji ambao pia wamekuwa wakishirikiana katika kazi zao. Kama unakumbuka Chidi alitoa wimbo ‘Get Down’ aliomshirikisha msanii huyo na sasa Nonini aka Godfather wa Genge ameamua kurudisha fadhila kwa kumshirikisha King Kong katika single yake mpya ya ‘Zipi Zoo’.

Zipizoo

Zipi Zoo ni single inayopatikana katika album ya ‘Mdundo za Kibiashara’ ya Nonini.

Godfather wa Genge anaitumia single mpya ‘Zipi Zoo’ kama majaribio ili kupata maoni ya mashabiki wake kujua mtazamo wao juu ya collabo ya yeye na Chidi Benz, na kama wanahisi ni sawa kwa wasanii hao wawili wakifanya album ya pamoja.

Katika email aliyoisambaza kwa vyombo vya habari Nonini ameandika:

“Prohabo is doing an experiment and we want your opinion about this Duo.

Mmoja toka Tanzania ChidiBeenz (King Kong) and Off course Nonini (Raprenuer), should this two guys do an Album Together. Remember Chidibenz featured Nonini on his single Get Down. Now Nonini has returned the favour and Featured Chidibenz on a brand new track from his latest album dubbed (Mdundo za Kibiashara). Sample the new single called Zipizoo and let me now what you think about this duo. “

Nonini amesema kuwa video ya Zipi Zoo inakuja pia.

Unamshaurije Nonini juu ya collabo yake na Chidi? Unahisi inafaa wafanye album ya kushirikiana? Andika maoni yako kwenye comments hapo chini.

Sikiliza Zipi Zoo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents