BurudaniHabari

Noorah hoi kwa Zai

NoorahMsanii Noorah a.k.a The Baba’z kutoka kundi la Chamber Squad ameweka wazi kuwa alichokielezea ndani ya ngoma ‘zai’  ni ukweli mtupu

NoorahMsanii Noorah a.k.a The Baba’z kutoka kundi la Chamber Squad ameweka wazi kuwa singo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘zai’ kuwa alichokielezea ndani ya ngoma hiyo ni ukweli mtupu, kwani ni kweli alimzimia ile kinoma lakini huyo demu alikuja akamzingua.

 

“Ni kweli nilimzimia sana huyo Zai na nilikuwa namfukuzia tangu tukiwa shule ya Sekondari Mazengo ambapo alinitangulia darasa moja, lakini pamoja na kumletea njaa zangu mtoto alimaliza shule na bado hakikueleweka kwani alitimua na kuniacha skuli, ndipo nikaamua kuandika ngoma hii ikiwa ni kama dedication kwake”-Nooarah

 

Ilikuwa ni mwaka 2000 ambapo mtoto Zai alimaliza Shule na mpaka 2004 Noorah kilikuwa kinamsokonyoa akilini ndipo akaamua kuandika ngoma hiyo ambayo ameshirikiana na Mwanafalsafah, imerekodiwa ndani ya studio za Home Boy za nchini Kenya.

 

Source: Bongo5

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents