Burudani

North West hataonekana katika TV show ya bibi yake, mama wa Kim Kardashian ‘KRIS’ kama ilivyoripotiwa mwanzo

Siku chache zilizopita vyombo vya habari viliripoti kuwa mtoto wa kike wa rapper Kanye west na Kim Kardashian ‘North West’ angetambulishwa rasmi kwa dunia kupitia kipindi kipya cha TV (talk show) cha mama mkwe wa Kanye ‘KRIS’ mwezi (July) kwa mujibu wa vyanzo vya karibu, lakini taarifa za sasa zinasema haitakuwa hivyo tena.

kim-kardashian and mom

Vyanzo vya karibu na mama North, Kim Kardashian vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa mpango wa Kim ni kuonekana na mwanae kwa mara ya kwanza katika picha. Mpaka sasa majarida mbalimbali yametangaza dau nono la mpaka $ 2million lakini Kim bado hajakubali offer yoyote.

Inasemekana Kim na Kanye hawapendi kabisa kumtumia mwanao kuingiza pesa, na Kim hana hata mpango wa kumuonesha katika msimu ujao wa reality show ya familia yake “Keeping Up with the Kardashians”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents