Habari

Noti ya 500 kuendelea kutumika hadi itakapotoweka mikononi mwa wananchi

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa noti ya Sh 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko, sambamba na sarafu ya Sh 500 hadi itakapotoweka mikononi mwa wananchi.

Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Marcian Kobello alitoa ufafanuzi huo kwa wananchi ili kuondoa uvumi ulioenea kuwa noti hiyo, haitatumika tena kuanzia Desemba 31, mwaka huu.

Alisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli, ni uvumi unaopaswa kupuuzwa na wananchi.

“Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi itakapotoweka mikononi mwa wananchi,” alisema.

Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti hiyo ya Sh 500, haitatumika tena kuanzia Desemba 31, mwaka huu.

Katika siku za karibuni sarafu ya Sh 500 zimekuwa nyingi, tofauti na zamani, hali inayoashiria kuwa ndio njia ya kuondoa noti hizo mikononi mwa wananchi.

Pia noti za Sh 500 zimekuwa zikikataliwa mara nyingi na abiria pamoja na makondakta katika mabasi ya umma, kutokana na mwonekano wake wa kuchakaa, hali inayosababisha majibizano kati ya abiria na kondakta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents