Michezo
Novack Djockovic ashinda taji la US Open
Novack Djockovic ambaye ni mchezaji namba moja wa tennis duniani ametwaa taji la Us Open baada ya kumshinda mpinzani wake Roger Federer anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani.
Novak amemshinda Federer kwa jumla kwa seti 6-4 5-7 6-4 6-4. Kwa ushindi huo mchezaji huyo ametwaa Grand slam ya tatu kwa mwaka huu.