Michezo

Novak Djokovic atolewa Australian Open na mchezaji mwenye kiwango duni

Mchezaji tennis, Novak Djokovic amekubali kipigo kutoka kwa mchezaji mwenye kiwango duni ambaye anashika nafasi ya 58 katika viwango vya ubora duniani, Hyeon Chung katika hatua ya nne ya michuano ya Australian Open.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Korean Kusini amemfunga Djokovic kwa jumla ya seti 7-6, 7-5, 7-6 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Grand Slam kwa mara ya kwanza katika historia yake ya tennis.

Djokovic ni mchezaji tennis mwenye mafanikio makubwa katika historia ya michuano hiyo na kufanikiwa kushinda Melbourne zaidi ya mara sita.

Lakini ameshindwa kushinda Grand Slam tangu mwaka 2016  katika michuano ya French Open kufuatia kusumbuliwa na majeraha na kiwango duni uwanjani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents