Michezo

Novak Djokovic atolewa katika mashindano ya Wimbledon

Novak Djokovic ametolewa katika mashindano ya Wimbledon baada ya kushindwa na raia wa Marekani Sam Querrey na hivyobasi kusitisha matumaini ya mchezaji huyo aliye nambari moja duniani kushinda taji la mwaka la Grand Slam.

Querrey,anaye shika nambari 28 katika mchezo huo, alishinda kwa seti 7-6 {8-6} 6-1 3-6 7-6 {7-5} katika raundi ya tatu baada ya mvua kusitisha mchezo kwa mda.
Ni mara ya kwanza kwa raia huyo wa Serbia kushindwa katika shindano kubwa tangu 2015 wakati wa fainali za French Open.

35E3EFF700000578-3671368-The_Serbian_tennis_star_makes_his_way_back_to_the_changing_room_-a-13_1467492035082

Djokovic alikuwa na matumaini ya kushinda taji lake la tatu mfululizo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 tayari ameshinda mataji ya Australia na Ufaransa mwaka 2015.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents