Michezo

Novak Djokovic atupwa nje French Open

Novak Djokovic ameyaaga mashindano ya mchezo wa tennis yanayo endelea huko mjini Paris, Ufaransa.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo ametupwa nje kwa jumla ya Seti 7-6 (7-5) 6-3 6-0 dhidi ya mchezaji Dominic Thiem katika hatua ya robo fainali.

Thiem ambaye ni raia wa Australia, sasa atakutana na Rafael Nadal katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa ulimwenguni baada ya kumtoa bingwa huyo mtetezi raia wa Serbia.

Mchezaji tenisi, Dominic Thiem akicheza na Novak Djokovic  katika michuano ya wazi ya Ufaransa 2017

Kwa upande wake, Nadal ametinga hatua ya nusu fainali baada ya kumto Mhispania Pablo Carreno Busta. Michezo hiyo ya hatua ya robo fainali ilichelewa kuanza kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.

Picha za Novak Djokovic baada kutolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa

BY HAMZA  FUMO

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents