Burudani

Nuh Mziwanda achimba mkwara mzito kwa Nawal, kisa?

Siku chache baada msanii wa muziki Bongo, Nuh Mziwanda kuweka wazi kuwa ameachana na Baby Mama wake, Nawal ametishia kuwa endapo ataona hamtunzi vema mwanae ataenda kumchukua.

Wawili hawa ambao walifunga ndoa na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye, Anyaghile hivi karibuni waliweka wazi kuachana na taarifa zilizopo ni kwamba bibie ameshaolewa tena.

“Mtoto still yupo na ningetamani sana kukaa naye tangu akiwa mdogo lakini nashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umri lakini nikiona mwanangu wanamfanyia vitu ambavyo si sawa nitaenda kumchukua na kukaa naye mimi mwenyewe,” Nuh ameiambia 5Selekt ya EATV na kuongeza.

“Kwa hiyo nampa muda nione, nikienda nikakuta mwanangu amenenepa, ana furaha, yupo poa ataishi naye mpaka umri utakapofika lakini nikienda nikakuta mwanangu amepungua nambeba na kuondoka naye,” amesema.

Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa Jike Shupa ameweka wazi kuwa wiki ijayo anatarajia kutoa ngoma mpya.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents