Burudani

Nuh Mziwanda ampa pole Shilole kwa kudundwa na Uchebe

Msanii wa muziki Nuh Mziwanda amelaani kitendo alichofanyiwa muimbaji na mjasiriamali, Shilole cha kupigwa na kuumizwa vibaya na aliyekuwa mume wake, Uchebe.

Nuh ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Shilole, ameandika ujumbe huu “Tuachane na mambo ya Nyuma Ila Nimesikitishwa sana na kitendo Cha kikatili kilichotokea kwako Zuwena ‘inasikitisha sana Kama Baba ambae nna mtoto wa kike pia Nawaza ingetokea kwa mwanangu ningejisikiaje ‘nimeishi na wewe takribani miaka minne sikuwahi kugusa mwili wako kwa mabavu ‘yote nilijua una family inakuangalia linaweza kutokea lolote ‘japo kukwazana inatokea sana Tena Mara kwa Mara Ila Kuna Aina ya kumpiga mwanamke na si kwa Aina ya upigaji uliopigwa ‘Nimeumia sana Kama Baba ambaye nna mtoto wa kike pia .Pole sana Zuwena Tunakuombea urudi kwenye hali yako 🙏 Hongera Sana Kwa Kusimama kuwakilisha wanawake wanaonyanyaswa na kukaa kimya 🤛”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents