Nurdin alalamikia kuonewa kisa chipukizi


Mwanamuziki anayechipukia Nurudin ameilalamikia kampuni moja ambayo imetengeneza video yake ya Kitorondo na kusema imemtia hasara kubwa. Nurudin alisema kwamba aliongea na kampuni hiyo na kuilipa fedha zile ambazo alizihitaji, lakini chaajabu producer alichukua fedha na kumfanyia pole pole na baadaye kuisusa kabisa.

Sikiliza Kitorondo hapa chini

Nurdin amesema ingawa alifanyiwa hayo yote, bado video yake ikaja kumaliziwa na mdogo wake ambaye pia alisema picha nyingi ambazo zilichukuliwa, ikiwemo ya mchekeshaji Mboto, hazikutokea ingawa alitumia fedha nyingi kufika huko, jambo ambalo angeambiwa asingeingia gharama hiyo.

Amesema matukio kama hayo huwa wanafanyiwa sana wasanii kama wao ambao wamekuwa wakitoka kwa mara ya kwanza, jambo ambalo linawakatisha tamaa na kuliona Game gumu kisa Maproducer hao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents