Habari

Nyalandu arudi nyumbani kugombea nafasi ya Ubunge

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu, ambaye Oktoba 30 mwaka 2017 alitangaza kujiuzulu ubunge na kuhamia Chama Cha Demnokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametangaza nia yake ya kurejea kwenye kinyang’anyiro cha cha kuwania ubunge wa jimbo hilohilo alilolitumikia kwa miaka 17 tangu mwaka 200-2017.

Hivi karibuni Nyalandu alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema ambapo kura hazikutosha hivyo akashinda Tundu Lissu.

Kupitia akaunti yake wa Twitter, Nyalandu ameandika; “Nitashiriki kama Mgombea katika kinyang’anyiro cha kumpata mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema Jimbo la Singida Kaskazini. Uchaguzi huo utafanyika leo, Jumatatu, Agosti 10, kijijini Ilongero. Asanteni sana kwa sala na dua zenu, na zaidi, kwa upendo wenu wa daima kwangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents