Michezo

Nyerere fc yajitoa daraja la 1

 

Timu ya Nyerere Fc ya Kilimanjaro iliyokuwa ikishiriki ligi ya daraja la kwanza Tanzania bara,imeshindwa kuendelea na ligi hiyo baada uongozi wa timu hiyo kusambaratika.


Akizungumza na Bongo5 kocha mkuu wa timu hiyo, Shungu Ramadhani, alisema timu hiyo ilitakiwa kwenda Mbeya kucheza mechi na Tanzania Prison juzi lakini ilishindikana.

Kocha huyo alisema timu hiyo ilijitoa kwenye ligi hiyo baada ya kuzuka kwa mgogoro baina ya viongozi wa timu hiyo.

Shungu alisema baadhi ya viongozi wa timu hiyo ni ccm na wengine chadema,hali iliyo sambaratika kwa timu.

Tunapata taabu sana, chakula ni shida, fedha hatuna ndio maana tumeshindwa kwenda Mbeya kucheza na Tanzania Prison yote hayo inatokana na viongozi wa timu hiyo kutokuelewana kutokana na itikadi zao za vyama,wapo CHADEMA na wengine CCM.

Kocha alisema wachezaji wote wamekwenda makwao,uongozi umegawanyika hivyo timu hiyo haitaweza kuendelea na kushiriki ligi daraja la kwanza msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents