Burudani

Nyimbo 4,000 zawasilishwa kwa Celine Dion baada ya kutangaza anahitaji kuandikiwa nyimbo mpya

Ombi la Celine Dion kuhusu kuandikiwa nyimbo kwaajili ya album yake mpya ya Kifaransa, limepokelewa kwa mafuriko ya nyimbo zilizowasilishwa.

celine_dion_press_pic_dl

Takriban nyimbo 4,000 zilitumwa kwenye website ya Dion na kampuni inayomsimamia hadi kufikia October 5.

Mume wa Dion, ambaye pia ni meneja wake, Rene Angeli na CEO wa kampuni ya Les Feeling Productions, Aldo Giampaolo walidai kushangazwa na muitikio huo mkubwa.

Mapema mwa mwezi August, muimbaji huyo alitangaza kuwa anapokea nyimbo mpya na kwamba mtu yeyote angeweza kushiriki.

Muimbaji huyo wa Canada, 47 na maarufu kwa wimbo wa ‘My Heart Will Go On’ uliotumika kwenye filamu ya mwaka 1997, Titanic, alisema anahitaji nyimbo mpya kwaajili ya album ya Kifaransa itakayotoka mwaka huu na nyingine ya Kiingereza itakayotoka mwaka 2017.

Nyimbo zilizowasilishwa sasa ni kwaajili ya album yake ya Kifaransa.

Jopo la watalaam wa muziki litakaa kuchuja nyimbo hizo hadi kufikia 25. Mashabiki watahusika pia kuchagua nyimbo 25 zitakazopita kupata zile zitakazoingia kwenye album yake na washindi kutangazwa December 1.

Album ya mwisho ya Dion ilitoka mwaka 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents