Burudani ya Michezo Live

Nyimbo mpya za Darassa tumeziandaa kama tunamwandaa Rais wa nchi – Hanscana

Mashabiki wengi wa muziki nchini wanataka kujua Rapa Darassa ambaye yuko chimbo atakuja na wimbo gani baada ya hit single yake ‘Muziki’.

Darassa bado yupo kwenye tour yake ya kimatifa nchini Rwanda na Burundi na baada ya hapo ataachia kazi yake mpya.

Akiongea na Bongo5, muongozaji wa video nchini, Hanscana ambaye ni meneja wa Darassa, amefunguka kuzungumzia ujio wa rapa huyo baada ya ‘Muziki’.

“Sisi tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua mashabiki wanataka nini,” alisema Hanscana. “Maandalizi ni makubwa sana, yaani ni kama tunaandaa Marais 5 wa nchi. Kwahiyo tumejipanga vizuri kuhakikisha jamaa anarudi vizuri katika game,”

Rapa huyo alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini ameshindwa kutokana na tour yake ya kimataifa.

Video ya wimbo ‘Muziki’ wa rapa huyo imeangaliwa mara 7,056,225 kwa kipindi cha miezi 5 tu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW