Habari

Nyimbo mpya za Michael Jackson ambazo hazikuwahi kusikika zitatolewa hivi karibuni

Ikiwa ni miaka 4 toka mfalme wa Pop duniani Michael Jackson afariki duniani, producer aliyehusika kuitengeneza album yake ya mwisho anategemea kuzitoa nyimbo na video za hit maker huyo wa ‘Thriller’ ambazo hazijawahi kusikika wala kuonekana.

King of Pop Michael Jackson dies at 50

Fred Jerkins III, producer aliyefanya kazi na MJ katika album yake ya (2001) ‘Invincible’ na pia ni mdogo wa producer Rodney Jerkens, ana mpango wa kutoa nyimbo na video za star huyo wa dunia marehemu Jackson ambazo hazikuwahi kutoka.

“There is a project in the making right now and that will include all of those songs.” Alisema Jerkins III wakati akizungumza katika chuo cha Access to Music kilichopo Birmingham, Uingereza.

FredJerkinsIII
Fred Jerkins III

Album ya kwanza ya MJ ‘Got to Be There’ ilitoka (January 1972) wakati album yake ya mwisho’ Invincible’ ilitoka (October 2001). Michael Jackson alifariki (June 25, 2009) katika hospitali ya UCLA Medical Center. Kifo cha MJ kilitokea wakati akijiandaa na ziara ya tamasha lake la ‘This Is It’ lililotegemewa kuanza katikati mwa mwaka 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents