AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Nyimbo za album ya ‘Money Mondays’ ya Vanessa Mdee zatajwa, Mastaa wakubwa duniani washirikishwa

Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee jana Jumatano Desemba 20, 2017, ameachia album yake mpya ya ‘Money Mondays’ ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na Watanzania pamoja na mashabiki wake duniani kote.

Album ya Money Mondays imehusisha mastaa wakubwa duniani kama Mohombi kutoka Sweden, Konshens kutoka Jamaica na Rapa namba moja barani Afrika, Cassper Nyovest na K.O wote kutoka Afrika Kusini.

Mohombi amesikika kwenye wimbo wa ‘Kwangu Njoo’ ambao ni namba 13 kwenye album hiyo, huku Rapa Cassper Nyovest akipata shavu kwenye wimbo wa ‘Pumzi ya mwisho’ ambamo yupo pia Rapa Joh Makini kutoka Weusi Kampuni.

Wasanii wengine waliopata shavu kwenye album hiyo ni Mr P, Reekado Banks wote kutoka Nigeria, G Nako, Tahpha, Tammy Flavour, Maua Sama na Jux.

Maproducer waliohusika kutengeneza nyimbo za album hiyo ni Nahreel, EKelly, S2Keez, Tahpha, Bob Manecky, Breezy na Lufah.

Album ya Money Mondays itaachiwa rasmi Januari 15, 2018 na kwasasa unaweza uka Pre-Order kabisa kabla haijatoka ingia HAPA .

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW