Burudani

Nyimbo za matusi zilitoka wakati wa kampeni – Nikki wa Pili

Bado mambo ni moto, ni baada ya serikali kuwafungia na kutoa onyo kwa baadhi ya wasanii ambao kazi zao zilionekana kwenda kinyume na maadali. Baada ya hatua hiyo ya serikali kumeibuka mjadala mpana kila kona.

Rapper Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi ameeleza kuwa kipindi cha kampeni (2015) kulikuwa na nyimbo nyingi ambazo zilikuwa kinyume na maadili. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika;

“Tukizungumzia nyimbo za matusi bwana zilitoka wakati wa kampeni, bwana we matusi ya nguoni, tena yakitukana watu wazima na heshima zao, hapa walezi walikaa kimyaaa,” amesema Nikki.

“Basata kama walezi wetu, msisahau pia kuyalinda maadili yetu ya kiuchumii, kama mlezi halafu watoto wako wanakuwa wanaishia kufa, inamanisha hawakulelewa vizuri kiuchumi,” ameongeza.

Hapo jana Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilimfungia kwa miezi sita msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki kutojihusisha na shughuli zozote za sanaa baada ya kukaidi agizo la kubadilisha maudhi ya wimbo wake wa Kiba_100, pia serikali ilitoa onyo kwa msanii Nay wa Mitego kutokana na mwenendo wake kisanaa kukiuka maadili..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents