Burudani

Nyimbo zangu sio ‘bubble gum’– Kala Jeremiah

Msanii wa Hip Hop nchini, Kala Jeremiah amesema muziki wake una uwezo wa kudumu kwa muda mrefu zaidi ndio maana hana haraka ya kutoa nyimbo kila mara.

Rapper huyo ameimbia Times FM kwa sasa ana mwaka mmoja tangu ataoe wimbo wake Wana Ndoto lakini bado muziki wake ni mkubwa na sasa yupo mbioni kutoa wimbo mpya.

“Nilikuwa najaribu kupima uwezo wangu umefika wapi kwa sasa na ni kwa sababu nyimbo zangu sio ‘bubble gum’, zinadumu muda mrefu, kwa hiyo nikataka nione je ninachokihisi ndio kilichopo?, yaani nyimbo zangu ninadumu kwa muda mrefu, kwa hiyo nimeprove ni kweli,” amesema Kala.

“Nilitoa wimbo wangu mwezi wa saba nikaamua kujipa mwaka mzima bila kutoa wimbo kuangalia nguvu yangu, unajua msanii sio lazima utoe wimbo kila siku, unaona watu kama wakina Jay Z heshima yao ni kubwa hata kama hawajatoa wimbo miaka miwili,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Kala amesema ukimya wake alikuwa anajipanga na mara baada ya kumalizika mfungo wa Ramadhan atatoa wimbo na hadi sasa nyimbo 10 zipo tayari ambazo amewashirikisha wasanii wa Bongo na mmoja kutoka nje.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents