Michezo

Nyoso ashushiwa adhabu kali na TFF

By  | 

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya  Nidhamu imemshushia adhabu kali mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kwa kosa la kumpiga shabiki baada ya mechi kati ya timu yake na Simba SC.

Juma Nyoso

Kamati hiyo ya TFF iliyokutana Jumamosi iliyopita Februari 10, 2018 imemfungia Nyoso mechi tano na kumpiga faini ya shilingi 1,000,000 (Milioni moja) baada ya kikao hicho kujiridhisha kuwa mchezaji huyo alimpiga shabiki huyo.

Soma zaidi – Juma Nyoso mikononi mwa polisi kwa kumtwanga shabiki

Nyoso alimpiga shabiki baada ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu yake ya Kagera Sugar dhidi ya Klabu ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments