Burudani

Nyota Ndogo awajibu wanaoteta kwanini hazeeki

By  | 

Staa wa kike wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Kenya maarufu kama Nyota Ndogo, amewajibu watu wanaoonekana kumfUatilia maisha yake binafsi.

Nyota ambaye alizaliwa mwaka 1981, amekuwa kwa game ya muziki tangia mwaka wa 2004 ambapo tokea hapo amekuwa akitoa hits za muziki kila anapoingia studioni kurekodi.

Muziki kwake umekuwa kila kitu, na si mara moja amekuwa akihoji kwenye vituo vya habari kuwa hata nyumba anayoishi kwa sasa imejengwa na pesa za muziki pamoja na biashara nyingine ambazo zinazidi kumtilia kipato cha kila siku.

Nyota ni baadhi ya mastaa wa muziki wa nchini Kenya wanaoheshimika sana, na pia amekuwa katika mstari wa mbele katika wale mastaa wakongwe nchini Kenya ambao hawakosi show kila wakati.

Hata hivyo mbali na mafanikio hayo, Nyota Ndogo katika maisha yake ya kawaida hakosi kupitia changamoto za kimaisha kama staa wengine Afrika. Leo kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nyota ametupia ujumbe unaonekana kuwasuta watu fulani wenye kupenda kumdadisi maisha yake binafsi hadi kufikia kiwango cha kumuuliza kwanini yeye hazeeki.

Naye mwanadada huyu, hajasita kuwajibu wanaouliza maswali kama haya kwa kuuandika ujumbe ulioambatana na picha yenye kumuonyesha akiwa na tabasamu kubwa kwenye kipaji chake cha uso…nikinukuu, Nyota ameandika: Wanasema why uzeeki nyota nawajibu nakubali matokeo and I smile all the time, sijui kukasirika kwa mda mrefu ila ikifikia hapo basi umeniumiza sana.”

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments