Nyota Ndogo azungumzia kuzushiwa Kifo


Mwanamuziki wa mjini Mombasa Kenya, Nyota Ndogo amelazimika kuzipoza hofu za familia yake, marafiki na mashabiki baada ya kuzushiwa kufariki dunia wiki hii.
Nyota ameliambia gazeti la The Star la Kenya, “Sikujua fununu hizi zilianzia wapi, kwasababu muda huo nilikuwa kwenye tamasha la Sawa Sawa Nairobi ambako nilikuwa.
Aliniambia kuwa amesoma kupitia Facebook kuwa nimefariki. Nilimwambia acomment kwenye post hiyo na aseme kuwa ameongea nami muda mfupi na kwamba yote ni uongo.”
Kutokana na simu hiyo ya jumapili hiyo, mwanamuziki huyo wa Watu na Viatu alianza kupokea simu nyingi kutoka kwa DJ’s, marafiki na hata kaka yake Juma alimuuliza kama yupo salama.
“Cha kuhuzunisha kuhusiana na hili ni kwamba mama yangu anaishi mbali na mimi, hivyo masuala ya uongo kama haya yakimfikia humpa wasiwasi sana. Husababisha madhara makubwa,” alisema. “Ningependa kuwaomba watu wathibitishe kwanza habari kabla hawajaisambaza. Ndio, kifo kipo kwa kila mtu, siogopi kufa lakini kwakuwa sijafa acheni kuniua.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents