Burudani

Nyota Ndogo wa Kenya ampa tano ex wa mumewe

By  | 

Kuna tofauti kubwa kati ya maisha ya wazungu na yetu sisi tunayoishi na familia zetu. Mwanaisha Abdalla maarufu kama Nyota Ndogo amethibitisha hilo kupitia mtandao wake wa Instagram.


Nyota Ndogo akiwa na aliyekuwa mke wa mumuwe Carina Nielsen

Muimbaji huyo kutoka Kenya, ameonyesha kushangazwa na maisha ya watu hao baada ya aliyekuwa mke wa mumewe, Carina Nielsen kumkubali zaidi mrembo huyo na kufikia hatua ya kumfundisha baadhi ya vitu yakiwemo mapishi.

“Yani wazungu wapo tafauti sana.huyu ni aliekua mke wa mume wangu.huyu ndie mwenye wale watoto wakubwa yani wapo na wajukuu na mume wangu.yani huyu aliponiona mara ya kwanza alinikumbatia na kuniambia karibu katika familia,” ameandika msanii huyo kwenye mtandao huo.

“Alinifunza kupika lazanya yani mwanamke mzuri sana.nae aliolewa kwengine pia yupo na watoto wakubwa uko alipo olewa @cbrandhoej you have the best mum in the world,” ameongeza.


Picha ya Nyota Ndogo akiwa na Mume wake Henning Nielsen wakati wa ndoa yao

Nyota Ndogo alifunga ndoa na mumewe raia wa Denmark, Henning Nielsen mwezi Mei mwaka jana.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments