Tia Kitu. Pata Vituuz!

Nyota wa filamu ya Om Shanti Om na Chennai Express, Deepika Padukone afunga ndoa 

Muigizaji wa filamu za Bollywood mwanadada, Deepika Padukone amefunga ndoa na Ranveer Singh katika hoteli moja ya kifahari nchini Italia siku ya Jumatano.

Image result for deepika padukone wedding

Nyota wa filamu za Bollywood mwanadada, Deepika Padukone (kushoto) akiwa na mumewe, Ranveer Singh ambaye pia ni muigizaji

Majina ya wapendanao hao yalienea kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter huku mashabiki wengi wakiwatakia heri.

Deepika Padukone ambaye alijizoelea umaarufu mkubwa hasa baada ya kushirikishwa kwenye filamu ya Sharukh khan inayojulikana kama Chennai Express na ile ya Om Shanti Om amewahi kuwa pamoja na mumewe Ranveer Singh katika filamu ya tatu zikiwemo Bajirao Mastani na Padmaavat ambazo zilipata bahati ya kuwa maarufu.

Image result for Chennai Express

Deepika Padukone akiwa na Sharukh khan kwenye filamu ya Chennai Express iliyotoka mwaka 2013

Jarida maarufu la Forbes liliripoti kuwa wanandoa hao wamepata faida ya dola milioni 21 katika kipato cha pamoja mwaka jana.

Harusi ilifanyika Jumatano, siku iliyo kumbukumbu ya walipoigiza filamu yao ya kwanza pamoja mnamo 2013 – Goliyon Ki Rasleela Ram-Leela.

Licha ya kwamba waandishi hawakualikwa kwenye harusi hiyo, picha za sherehe za kabla ya harusi zilifichuka katika majarida ya burudani na magazeti.

Watu wamekuwa wakizitafuta picha hizo pakubwa ambazo huenda zimesambazwa na wageni waliohudhuria sherehe katika mitandao yao ya kijamii – inaarifiwa wapenzi hao waliwapiga marufuku wageni waalikwa kuweka chochote kuhusu harusi hiyo katika mitandao.

Uvumi kuhusu kuchumbiana kwa waigizaji hao nyota ulianza kusambaa miaka 6 iliyopita, lakini hawakulithibitisha hilo wazi mpaka mapema mwaka huu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW