Tupo Nawe

Nyota wa Wolfsburg ajeruhiwa usoni

Jeraha la Yannick ni pigo kubwa kwa Wolfsburg wakati huu timu hiyo ikijiandaa kujiimarisha na Bundesliga itakayoanza kutimua vumbi tena Mei 16.

Kiungo wa Wolfsburg Yannick Gerhardt amepata jeraha baya usoni baada ya kugongana kichwa na mchezaji mwenzake na kupasuka wakati wa mazoezi.

Jeraha hilo lilitokea wakati wa mechi ya mazoezi ya vikosi viwili vya wachezaji 11 kwa 11.

Kocha Oliver Glasner alisena katika mkutano wa waandishi wa habari kwa njia ya video kwamba kujeruhiwa kwa Gerhardt ni pigo kubwa kwa klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amelazwa hospitali na lazima afanyiwe upasuaji.

Madaktari wa vilabu vya Ujerumani walionya awali kwamba huenda kukatokea ongezeko la majeraha kufuatia miezi miwili ya ligi kusimama.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW