Habari

Nyota Yako inatoka Msumbiji?

Said ComorienWimbo ambao unavuma kwa kasi wa msanii TID ‘Nyota Yako’ ambao unatamba sana Tanzania nzima inasemekana kuwa prodyuza huyo ametumia biti ya msanii Pasada wa nchini Msumbiji na kujifanya kuwa ameitengeneza yeye. Sikiliza nyibo zote mbili hapa!

Said Comorien na TID


Wimbo ambao unavuma kwa kasi wa msanii TID ‘Nyota Yako’ ambao umetengenezwa katika studio za Metro jijini Bongo inasemekana kuwa prodyuza huyo ametumia biti ya msanii Pasada wa nchini Msumbiji na kujifanya kuwa ameitengeneza yeye.


Kitendo hiki kimesababisha kuvuma kwa maneno mbali mbali hadi kupelekea kufukuliwa kwa hili linalodai kuwa biti hiyo hiyo alipewa pia msanii Ismail aliyekuwa Soul n’ Faith ambapo ameshaitumia na kurekodi singo yake inayokwenda kwa jina la ‘Khadija’


Imekuwa ndio wimbo wa taifa katika vituo mbali mbali vya redio na vipindi vya burudani kwa kitendo hicho ambacho kinaonekana kumshushia hadhi sana prodyuza huyo japo yeye amekuwa akikanusha vikali kuwa hajaiba ila hata kiziwi ukimsikilizisha ngoma hiyo atasema jamaa amecopy na kupaste.


Uchunguzi bado unaendelea kumpata TID, Ismail na Said Comorian ili kujua nini Hatma ya sakata hilo kwa mpaka dakika hii, prodyuza Said imesahaulika kama amewahi kufanya kazi zilizompatia sifa na kuwatoa wasanii kibao akiwemo Ray C na ‘sogea sogea’ na mikono kibao ambayo imekaa kwenye chati mbali mbali za hapa nchini.


TID “Nyota Yako”
{play}tid_nyota_yako.mp3{/play}


Wimbo wa Pasada kutoka Msumbiji
{play}pasada_nyota_yako.mp3{/play}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents