Nyumba ya 50 Cent yateketea

Mjengo wa maana uliokuwa unamilikiwa na mwanamuziki 50 Cents huko Long Island ndani ya jiji la New York nchini Marekani umeteketea vibaya na uharibifu wa mali nyingi umetokea lakini watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wamesalimika.

Nyumba ya 50 Cent yateketea

 

Mjengo wa maana uliokuwa unamilikiwa na mwanamuziki 50 Cents huko Long Island ndani ya jiji la New York nchini Marekani umeteketea vibaya na uharibifu wa mali nyingi umetokea lakini watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wamesalimika.

 

Katika kisanga hicho alikuwemo aliyekuwa mchumba wa rapa 50 Cent pamoja na mtoto wake lakini majina ya watu wengine wanne waliokuwepo ndani ya nyumba hiyo hayakuweza kupatikana haraka.

 

Inasemekana watu hao hawakupata majeraha yeyote ila waliwahishwa haraka hospitalini baada ya kuathirika na hewa chafu waliyokuwa wakivuta ya wakati wakiwa ndani ya mjendo huo uliokuwa ukifuka moshi sana.

 

Wakili wa mchumba wa zamani wa mwanamuziki huyo aliyejulikana kwa jina Shanique alisema alikuwa anaishi ndani ya nyumba hiyo akiwa na watoto wake wawili, mmoja akiwa ni mtoto wa rapa 50 Cent na pamoja na wafanyakazi wake sita.

 

Vilevile wakili huyo aliendelea kubainisha ya kwamba mpaka sasa hawajajua chanzo cha moto huo ila wapo kwenye upelelezi wa kujua na taarifa zitatolewa.

 

Halikadhalika kuhusiana na habari hii msemaji mkuu wa 50 Cent alisema ya kwamba rapa huyo anashukuru Mungu kwamba watu wote ndani ya nyumba hiyo wametoka wakiwa saalama na hajali kuhusu uharibifu wa nyumba hiyo.

 

“Anashukuru sana kwamba kila mmoja ndani ya nyumba hiyo ametoka salama pamoja na mtoto wake wa pekee Marquis alitoka kwa umakini” Msemaji huyo alisema.

 

Polisi inaendelea na upelelezi kuhusiana na suala hili na habari zitawekwa wazi wakishamaliza upelelezi juu ya chanzo cha moto huo.

 

 

Nyumba ya 50 Cent yateketea
Nyumba ya 50 Cent kabla ya tukio

 

 

Nyumba ya 50 Cent ikiwaka moto
Nyumba ya 50 Cent ikiteketea

 

 

Nyumba ya 50 Cent baada ya tukio

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents