HabariUncategorized

Nyumba ya familia ya GUPTA yenye ukaribu na Rais Jacob Zuma yazingirwa na polisi

Askari Polisi mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini wameizingira nyumba ya familia ya kitajiri ya ‘Gupta’ ambayo ipo na mahusiano ya karibu na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Picha inayohusiana
Rais Jacob Zuma akiwa na baadhi ya wanafamilia ya kifahari ya GUPTA.

Kwa mujibu wa mtandao wa Reuters umedai kuwa polisi wamezingira barabara zote zinazoingia kwenye eneo la nyumba za familia hiyo huku wakiwa na silaha nzito za kijeshi.

Msemaji wa jeshi la polisi mjini  Johannesburg, Hangwani Mulaudzi amethibitisha taarifa hizo lakini amekataa kutolea maelezo kwa nini nyumba hiyo ya kifahari imezingirwa na polisi.

Tangu mwaka 2015 familia ya Gupta imekuwa ikishutumiwa na viongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini kuwa inahifadhi mali za wizi zinazoibwa serikalini na Rais Zuma.

Ulinzi huo umekuja katika kipindi hiki ambacho Chama cha ANC kwa sauti moja kimetoa tamko la kumshinikiza Rais Jacob Zuma kujiuzulu nafasi yake ya urais.

Jana chama hicho kilimpa masaa 48 Rais Jacob Zuma kujiuzulu urais huku mwenyewe akitaka apewe muda wa miezi mitatu hadi sita kuchukua uamuzi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents