Shinda na SIM Account

Nyumba ya Mjane yapigwa mnada kwa dk 5 wakati mwenyewe hajui chochote (Video)

Mama mjane ambaye ni mama wa watoto watatu amejikuta katika wakati mgumu Ijumaa hii baada ya kuamka asuburi na kukuta nyumba yake iliyopo kwenye ploti namba 239 Block B mtaa kwa Kondo, Mbezi, ikipigwa mnada na kampuni ya Nkaya Company bila kuwa na taarifa yoyote.

Mama huyo ambaye anatambulika wa jina la Benadetha Ruyendela, amedai sehemu hiyo ya kiwanja aliyojenga aliinunua kutoka kwa Bi. Zainabu J Kaswaka na dokomenti zote anazo.

“Kusema kweli sina jinsi kama mnavyoniona mimi ni mjane, hii nyumba ambayo imepigwa mnada kimagumashi ni yangu. Mwaka 2014 nilitafuta kiwanja na baadaye nikakutana na huyo Zainabu, akaniambia mimi nakiwanja changu nikuuzie chote nikasema sina pesa, akasema basi ngoja nikukatie sehemu ya hiyo pesa uliyonayo ndio akanikatia hii sehemu iliyoijenga na ikaweka ukuta kama fensi kabisa. Sasa juzi nimeshangaa wamekuja watu wakapiga mnada nyumba yangu wakati mimi sijui chochote,” alisema Benadetha.

Aliongeza, “Baada ya kuona hivyo nikampigia Zainabu kumweleza yote, akaniambia anakuja kweli dakika kadhaa akawa amefika, wakati anafika tayari wale waliopiga mnada nyumba wameshaondoka na wamenipa siku 30 nihame. Zainabu baada ya kufika eneo la tukio akazungumza na waandishi wa habari ambao walikuwa pale akasema suala la mgogoro wa kiwanja liko makamani na tayari mahakama iliweka zuio. Sasa mimi nimeona nizungumze na waandishi wa habari kumuomba Mhe RC Makonda anisaidie, mimi ni mjane, nimeingizwa tu kwenye hili sakata, nitaenda wapi baada ya kufukuzwa jamani,”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW