Habari

Nyumba ya Mwalimu Nyerere kuvunjwa

NYUMBA ya Mwalimu Nyerere ya Magomeni jijini Dar es Salaam ambayo ni sehemu ya makumbusho ya Taifa inatarajiwa kuvunjwa ili kuruhusu mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa la biashara utakaosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Watu wakipita karibu na nyumba ambamo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliishi eneo la Magomeni Dar es Salaam, jana. (Picha na Athumani Hamisi).Gloria Tesha


NYUMBA ya Mwalimu Nyerere ya Magomeni jijini Dar es Salaam ambayo ni sehemu ya makumbusho ya Taifa inatarajiwa kuvunjwa ili kuruhusu mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa la biashara utakaosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).


Nyumba hiyo ambayo ipo karibu na barabara ya Morogoro, Mtaa wa Morogoro na Ruaha aliishi Mwalimu wakati wa harakati za kutafuta Uhuru wa Tanganyika mwaka 1956 hadi 1960 na hivyo inatambulika kwa mujibu wa sheria kuwa miongoni mwa kumbukumbu za Taifa.


Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ya Juni 11 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, John Kimario, mwaka huu kwa wapangaji hao, inakiri kuwa Idara ya Mambo ya Kale iliyo chini ya Wizara hiyo ndio wasimamizi wa rasilimali zote za urithi wa utamaduni na kumbukumbu kwa mujibu wa sheria ya Mambo ya Kale na 10 ya mwaka 1964 na marekebisho namba 22, 1979.


Aidha barua hiyo (nakala tunayo) inaeleza kuwa kupitia sheria ya kuwaenzi waasisi wa Taifa namba 8 ya mwaka 2004, Ibara ya III, kifungu cha 10 (i) na 11 (i) inampa mamlaka Mkurugenzi wa Nyaraka za Taifa kuvitambua na kuviweka kwenye orodha ya kuhifadhiwa mali na vitu vyote vya waasisi wa Taifa.


Kubomolewa kwa nyumba hiyo yenye wapangaji sita kutafanyika mara baada ya wapangaji hao kuhama ifikapo Juni 30, mwaka huu baada ya notisi ya miezi sita waliopewa na NHC, Desemba mwaka jana iliyoanza kutekelezwa Januari mwaka huu.


Uvunjwaji wa jengo hilo umeibua mgogoro kati ya wapangaji ambao baadhi yao wameishi hapo kwa zaidi ya miaka 30 na NHC kwa kile kilichodaiwa kuwa ujenzi wa jengo hilo la kisasa utaharibu uhalisia wa jengo hilo.


Mkurugenzi wa Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa, Peter Mlyansi, alipoulizwa kuhusiana na jambo hilo jana, alikiri kupata barua, lakini alisema idara yake haihusiki na uvunjwaji wa jengo hilo bali Makumbusho ya Taifa na Idara ya Mambo ya Kale.


Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema jengo hilo kama lipo katika hifadhi ya mambo ya kale ya Taifa linapaswa kuwa sehemu ya kumbukumbu ya nchi.


Akizungumza kwa niaba ya wapangaji hao, mmoja wa wapangaji hao ambaye pia ni Mjumbe wa Nyumba Kumi, Ramadhani Shaban alisema wanaiomba serikali kutoa kauli moja kuhusiana na uhalali wa nyumba hiyo kuvunjwa kwa lengo la kuifanya ya kibiashara.


“Tunawasiwasi kwamba NHC wanatufukuza sisi wafanye biashara katika jengo hili, sisi tunaona ni makosa serikali lazima itizame jambo hili hapa aliishi Nyerere akigombea uhuru na pako vile vile tutawaeleza nini wajukuu zetu kama kumbukumbu hizi zinapotea?” alihoji Shaban.


Souce: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents