Nyumba ya Nas yapigwa mnada baada ya kushindwa kulipa mkopo

Mambo yanaonekana kumwendea kombo rapper Nas baada ya mtandao wa TMZ kuripoti kuwa mjengo wake wa kifahari wa jimboni Georgia umepigwa mnada.

Kwa mujibu wa rekodi rasmi, Nas alinunua nyumba hiyo mwaka 2004 kwa $585,000 lakini kwa mujibu wa SunTrust bank ambayo ilimpa mkopo Nas alishindwa kuulipa na sasa anadaiwa $507,000.

SunTrust hivi karibuni iliishikilia nyumba hiyo na kuiuza kwa mnada mwezi uliopita kwa dola 348,500 ikiwa chini kabisa ya bei aliyoinunulia nyumba hiyo miaka nane iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents